Author: Fanny Crosby Hymnal: Mwimbieni Bwana #73 (1988) Refrain First Line: Bwana vuta, vuta Lyrics: 1 Ni wako wewe, nimekujua
Na umeniambia,
Lakini Bwana, nataka kwako
Nizidi kusogea.
Refrain:
Bwana vuta, vuta
nije nisogee
sana, kwako mtini.
Bwana vuta, vuta,
Nije nisogee,
Pa damu ya thamani.
2 Niweke sasa nikatumike
Kwa nguvu za neema;
Uyapendayo nami nipende,
Nizidi kukwandama. [Refrain]
3 Nina furaha tele kila saa
Nizungumzapo kwako.
Nikuombapo nami napata
Kujua nia yako. [Refrain]
4 Mapenzi yako hayapimiki,
Ila ng'ambo yaliko.
Anasa pia sitazijua,
Bila kufika kwako. [Refrain]
Topics: Epifania, Mission Languages: Swahili
Ni wako wewe, nimekujua