268. Ni wako wewe nimekujua

1 Ni wako Wewe, nimekujua,
Na umeniambia;
Lakini Bwana, nataka kwako
Nizidi kusogea:

Refrain:
Bwana vuta, vuta,
nije nisogee sana
kwako mtini.
Bwana vuta, vuta,
nije nisogee
pa damu ya thamani.

2 Niweke sasa nikatumike
Kwa nguvu za neema;
Uyapendayo nami nipende
Nizidi kukwandama: [Refrain]

3 Nina furaha tele kila saa
Nizungumzapo kwako,
Nikuombapo, nami napata
Kujua nia yako: [Refrain]

4 Mapenzi yako hayapimiki
Ila ng'ambo yaliko.
Anasa pia sitazijua,
Bila kufika kwako: [Refrain]

Text Information
First Line: Ni wako Wewe, nimekujua
Title: Ni wako wewe nimekujua
English Title: I am Thine, O Lord, I have heard Thy voice
Author: W. H. Doane
Refrain First Line: Bwana vuta, vuta
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kumtambikia Mungu: Kumsifu na kumwomba Mungu
Notes: Sauti: I am Thine, O Lord, I have heard Thy voice by F. J. Crosby, Sacred Songs and Solos #607
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us