Text: | Kukichwa watu wote |
Author: | P. Gerhardt, 1607-1676 |
1 Kukichwa watu wote
walala, ng'ombe wote
na mbuzi na ndege.
Ee moyo wangu, sasa
uanze kufikiri
vinavyompendeza Mungu.
2 Jua limeingia,
Giza limetokea,
usiku karibu.
Jua lingine sasa
lang'aza moyo wangu:
Ni Yesu, Mwokozi wangu.
3 Miguu hata mikono
inafurahi sana,
kazi imekwisha.
Nao moyo wataka
kukombolewa hivyo
katika nguvu za mwovu.
4 Nafumba macho yangu,
nalala usingizi,
sijui lolote.
Wewe uangalie
roho na mwili wangu,
uliye mlinzi wetu mkuu.
5 Yesu furaha yangu,
unifunike sasa,
unikumbatie.
Uagiza malaika
wanikingie shida;
Shetani akinitaka.
6 Hata wapenzi wangu
nawaombea wote
wasione shida.
Mungu atawalinda
kwa jeshi la malaika
walale wote kwa raha.
Text Information | |
---|---|
First Line: | Kukichwa watu wote |
Title: | Kukichwa watu wote |
German Title: | Nun ruhen alle Wäđer |
Author: | P. Gerhardt, 1607-1676 |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Kumtambikia Mungu: Nyimbo za Jioni |
Notes: | Sauti: Nun ruhen all Wälder, Posaunen Buch, Erster Band #44 |