200. Mwenzetu, kazi yako

1 Mwenzetu, kazi yako
imekwisha duniani.
Umekwisha kutua
mzigo wa shida na taabu.
Yesu tupe kufika
walipo washindaji.

2 Yesu ni kiongozi
katika bonde la kufa.
Amekutangulia
kaburini na peponi.
Yesu tupe kufika
walipo washindaji.

3 Wewe wachukuliwa
na malaika kwa Mwokozi.
Utapokewa sasa
na wateule wa Mungu.
Yesu tupe kufika
walipo washindaji.

4 Mwili wako wazikwa,
ugeuke kuwa vumbi.
Twatumaini kwamba
ufufuko utakuwa.
Yesu tupe kufika
walipo washindaji.

5 Sasa unapandwa tu
kama mbegu ya shambani.
Mpaka yaje mavuno
siku ya kufufuliwa.
Yesu tupe kufika
walipo washindaji.

Text Information
First Line: Mwenzetu, kazi yako
Title: Mwenzetu, kazi yako
Author: Hajulikani
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kufa na kuzikwa
Notes: Sauti: Posaunen Buch #29, Nyimbo za Kikristo #153
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us