1 Sijui saa ya kufa kwangu,
maisha yangu yapita.
Naomba: Mungu,
Bwana wangu
kwa ajili ya Mwanao.
Shika roho yangu,
kwa furaha,
niache ulimwengu huu.
2 Tukiwa hapa duniani
kufa kunatuvizia,
hakutuwekei kiaga,
hunakuja kwa haraka.
Shika roho yangu,
kwa furaha,
niache ulimwengu huu.
3 Unifundishe nifikiri
vizuri mambo ya kufa,
nijutie makosa yangu,
yaondolewe na Yesu.
Shika roho yangu,
kwa furaha,
niache ulimwengu huu.
4 Unipe nguvu, nijiweke
tayari kwa mambo yote,
niweze kuitikia vema,
ukiniita kwa kufa.
Shika roho yangu,
kwa furaha,
niache ulimwengu huu.
5 Baba, ondoa dhambi zangu
kwa damu ya Bwana Yesu,
najificha katika huyu,
kwani amenikomboa.
Shika roho yangu,
kwa furaha,
niache ulimwengu huu.
6 Nikiwa naye Bwana Yesu,
sioni hofu kwa kufa.
Na saa ya kufa ikifika,
namtumaini Yesu tu,
Ninajua: Kwa damu ya Yesu
napata kufa kuzuri.
Text Information | |
---|---|
First Line: | Sijui saa ya kufa kwangu |
Title: | Sijui saa ya kufa kwangu |
German Title: | Wer Weiss wie nahe mir mein Ende |
Author: | A. J. v. Schwarzburg-Rudolstadt, 1637-1706 |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Kufa na kuzikwa |
Notes: | Sauti: Wer weiss wie nahe mir mein Ended, Asili: F. V. Buttstedt 1744, Posaunen Buch #68 |