Text: | Bariki yote yawe mema |
Author: | Mch. Sila Mzangi |
1 Bariki yote yawe mema
Yote yawe mbaraka.
Watu wa nchi za dunia,
Uwajaze utukufu.
Refrain:
Kaa kwetu, Bwana, bariki.
Uamini, wee ee ndugu
Kweli yake Kristo.
Jaa utukufu wa Bwana
siku zako zote
Vaa Mwokozi ee na kweli
yake, Haleluya.
2 Nyumba za wote zibariki
Kwa jina lako takata.
Ujaze utukufu wako,
Nchi zote za dunia. [Refrain]
3 Nyosha mkono, ubariki
Waliojiunga nawe.
Wakupokee maishani,
Watunzwe nawe milele. [Refrain]
4 Bwana, yatunze mambo yote
Yaliyo mazuri kwako.
Uwape wote wakuombao
Wafanikishe maisha. [Refrain]
Text Information | |
---|---|
First Line: | Bariki yote yawe mema |
Title: | Bariki yote yawe mema |
Author: | Mch. Sila Mzangi |
Refrain First Line: | Kaa kwetu, Bwana, bariki |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Ndoa |
Notes: | Sauti: Tumshangilies Mungu #95 |