1 Ukimpata mwenye moyo
Mwaminifu daima,
Umepata kito bora,
Wajaliwa na Mungu
Japo nimo shidani,
Hali yangu ya heri.
2 Ukiingiwa na taabu
Na kupatwa na msiba,
Mwenzi wako mwaminifu
Atakutia moyo.
Japo nimo shidani,
Hali yangu ya heri.
3 Haja yake mwenzi huyu
Kukusaidia tu.
Taabu yako ndiyo yake,
Hakuachi msibani.
Japo nimo shidani,
Hali yangu ya heri.
4 Rafiki za duniani,
Mali zitapotea,
Mwenzi wako mwaminifu
Atakaa kwa mpenziwe.
Japo nimo shidani,
Hali yangu ya heri.
5 Mtu kuwa na mwenzake
Mwaminifu daima,
Ndiyo hali duniani
Ipitayo kabisa.
Japo nimo shidani,
Hali yangu ya heri.
Text Information | |
---|---|
First Line: | Ukimpata mwenye moyo |
Title: | Ukimpata mwenye moyo mwaminifu |
German Title: | Ein getreuens Herzen wissin |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Notes: | Mtungaji wa wimbo: Jos Gersbach, Tumwimbie Bwana #78 |