188. Uchunguze ndani yangu

1 Uchunguze ndani yangu,
Iwe safi nia,
Kwangu kama kwako Mungu,
Idhihiri pia.

2 Uchunguze moyo wangu
Unifunulie,
Yaliyomo ndani yangu
Nami niyajue.

3 Kwanza washa zako tambi,
Kumefunga giza,
Nijue ambavyo dhambi
Ni za kuchukiza.

4 Uchunguze na mawazo,
Ni mbegu za mambo,
Asili ya machukizo,
Maumbuo-umbo.

5 Uzidi kuyachunguza
Katikati yangu
Hata uishe nifundisha
Udhaifu wangu.

6 Hapo nikikuinamia
Mbele zako, Mungu.
Hakika nitakujua
Ndiwe Mpenzi wangu.

Text Information
First Line: Uchunguze ndani yangu
Title: Uchunguze ndani yangu
English Title: Search me, O God, my actions try
Author: Assa Hull
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Chakula cha Bwana
Notes: Search me, O God, my actions try by F. Bottome, Sacred Songs and Solos #587
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us