154. Ondokeni! Tunaitwa

1 Ondokeni! Tunaitwa
na walinzi wa juu mnarani
Yerusalemu, amka wee!
Ni usiku wa manane,
yuaja Bwana wa arusi,
wanawali wako wapi?
Amkeni upesi!
Kaziwasheni taa.
Haleluya!
Fuateni arusini
kwenda kumpokea Bwana!

2 Sayuni ansikia,
moyo waruka kwa furaha,
yu macho anaondoka.
Mponya wake anashuka
mbinguni mwenye utukufu,
aleta mwanga wa kweli.
Taji yake yaja
na mwana wa Mungu.
Hosiana!
Twafuata kwenye shangwe
takale karamu yake.

3 Waimbiwa nyimbo nzuri
kwa misemo ya watu wote
na ya malaika mbinguni.
Tukifika mjini kwako
kwenye milango ya malulu
tutakuimbia nasi.
Furaha kama hii
haijasikiwa duniai.
Nasi sasa tunaimba,
tunakusifu, ee Bwana.

Text Information
First Line: Ondokeni! Tunaitwa
Title: Ondokeni! Tunaitwa
German Title: Wachet auf, ruft uns die Stimme
Author: Ph. Nicolai (1599)
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Yesu anatungojea mbinguni
Notes: Sauti: Wachet auf, ruft uns die Stimme by Ph. Nicolai, 1599, Posaunen Buch #52, Reichs Lieder #599
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us