127. Roho Matkatifu uje

1 Roho Mtakatifu uje
utujalie na sisi,
fanya makao kwetu.
Utupe nuru ya mbingu,
ung'aze mioyo yetu,
tumtumikie Mungu.
Uje, lete utukufu
na furaha na uzima;
haya twatafuta kwako.

2 U chemchem yenye
rehema,
unatunywesha hekima,
watufundisha vema,
tujue kuwaambia
wenzetu wasiojua
habari za wokovu.
Roho zetu uzifunge,
tuyatende mamo mema
wewe utukuzwe sana.

3 Umande mzuri wa mbingu,
geuza mioyo yetu,
tujae pendo lako.
Tupendane na wenzetu,
tuwafanyie mema tu
na kweli watu wote.
Kwetu uwe upendano:
kugombana kuwe mbali,
tuwe wa amani daima.

4 Ututakase mioyo,
utupe nguvu rohoni,
tushike mwendo mwema.
Tusifuate kiburi,
tamaa mbaya a mwilini
na mambo ya dunia.
Roho zetu ziongozwe
zifikiri mambo yako,
mpaka tufikapo kwako.

Text Information
First Line: Roho Mtakatifu uje
Title: Roho Matkatifu uje
German Title: O Heiliger Geist kehr bei uns ein
Author: M. Schirmer, 1606-1673
Publication Date: 1988
Topic: Yesu anawapa wanfunzi wake Roho Mtakatifu
Notes: Sauti: O Heiliger Geist kehr bein uns ein, Namba 121, Posaunen Buch, Erster Band #73, Lutheran Book of Worship #43
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us