109. Haleluya, Haleluya

1 Haleluya, Haleluya, Sauti
na mioyo juu,
tumwimbie Mungu nyimbo,
tumsifu na furaha.
Aliyemwaga damuye
kwa ulimwengu wote,
amefufuka ufuni sasa Yesu
Mwokozi.

2 Minyororo yake kifo
imekatika pia,
na katika watu wote
yee mzaliwa wa kwanza.
Yesu ameshinda sasa, nasi
twashinda naye.
Ametupatia nasi uzima wa
milele.

3 Kristo afufuka kwanza
nao wengi baadaye.
Atakapokuja tena,
watatokea naye,
mavuno yatakuwako mwisho
wa ulimwengu,
watafika furahani
wote watkatifu.

4 Mwokozi amefufuka,
nasi tutafufuka.
Tunyeshee kama mvua
neema yako ee Bwana.
Tutafute yaliyo juu,
siyo ya ulimwengu,
na uzima tutapewa
naye kristo kwa Mungu.

5 Tumsifuni, tumsifuni
Mungu wetu, apaswa.
Tumsifuni na Mwokozi,
aliyeshinda vita.
Tumsifuni naye Roho,
kisima cha mapenzi
Tumsifuni Mungu wetu,
ni Utatu wa enzi.

Text Information
First Line: Haleluya, Haleluya
Title: Haleluya, Haleluya
English Title: Hallelujah, Hallelujah!
Author: C. Wordsworth, 1807-1885
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Yesu amefufuka
Notes: Sauti: Sanctuary by J. B. Dykes, 1823-1876, Hymnal Companion #214, Nyimbo za Kikristo #86
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us