1 Usiku ulipotolewa,
Yesu, umetugawia
mapato ya mateso yako,
tukumbuke kufa kwako.
Waaminio wakusifu
wakija karamuni kwako.
2 Tunakumbuka kufa kwako,
tukila mwili wako huu;
twapewa nguvu ya uzima
tukinywa damu yako hii.
Karamu hii tunayopewa
yatuonyesha pendo lako.
3 Huu mkate ni chakula kweli,
hii damu yatutuliza;
mioyo yetu yapumzishwa
tukila mezani kwako.
Tunaongezwa nguvu zetu,
za kukutegemea vema.
4 Twahirikiana nao wote
walio viungo vyako;
kwani tunashibishwa sote
kwa mwili na damu moja.
Tu kundi la mchungaji mmoja,
kwa hivi twapatana sote.
5 Twapewa mwili wako Bwana,
tujue kweli ya kwambaa
miili yetu ya unyonge
itageuka vizuri.
Tutapokea mwisho kwako
miili mipya ya uzima.
6 Watupa mema mengi Bwana
Mwana Kondoo wake Mungu
mwenyewe u chakula chetu,
kweli twatunzwa vizuri.
Twakila hapa kwa uchungu,
lakini kwako kwa furaha.
Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #182