Upendo wa Mungu wetu

Upendo wa Mungu wetu

Author: Hermann Windolf
Published in 1 hymnal

Representative Text

1 Upendo wa Mungu wetu
ndio jua letu.
Hutung'azia moyoni
hufuta uchungu.
Giza hukoma na mchana
hutokea sasa,
furaha tupu na shangwe
huwamo moyoni.
Upendo huu
una nguvu
tangu mwanzo
na daima,
atupenda
mimi nawe,
tuwe karibu na yeye.

2 Tangu mwanzo
Baba Mungu
alivyotuumba,
ametuonyesha pendo
kwa kutukumbuka.
Hutupa mema mengi mno
duniani petu,
ila sisi hatukumpa
shukrani ya kweli.
Upendo huu
una nguvu
tangu mwanzo
na daima,
atupenda
mimi nawe,
tuwe karibu na yeye.

3 Ndipo akamtuma Yesu
mwenye pendo jingi.
Awaza pendo la kufa,
watalikubali.
Atuamsha atuita:
Acheni mabaya!
Tumjue anavyopenda
kutupa uzima.
Upendo huu
una nguvu
tangu mwanzo
na daima,
atupenda
mimi nawe,
tuwe karibu na yeye.

4 Nasi tudumu pendoni
Yesu Bwana wetu
Yeye jua la Baraka
Mioyoni mwetu
Tumwamini na tumpende
sasa na milele.
Amani tupu, rehema
zatoka kwa Yesu.
Upendo huu
una nguvu
tangu mwanzo
na daima,
atupenda
mimi nawe,
tuwe karibu na yeye.


Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #195

Author: Hermann Windolf

(no biographical information available about Hermann Windolf.) Go to person page >

Text Information

First Line: Upendo wa Mungu wetu
German Title: O Liebe goldner Sonnenstrahl
Author: Hermann Windolf
Language: Swahili
Notes: Sauti: O Liebe goldner Sonnestrahl by W. J. Baltzell, 1832-1893, Reichs Lieder #235, Nyimbo za Kikristo #150

Instances

Instances (1 - 1 of 1)
TextPage Scan

Mwimbieni Bwana #195

Suggestions or corrections? Contact us