1 Umejengwa juu Yerusalemu,
ninakutamani.
Moyo wangu ukikutamani,
wataka kupita
milima a mabonde,
kuruka kama tai
uache uliwengu
uingie kwako.
2 Siku nzuri!
Ninaingojea, ifike upesi.
Niiache dunia, niende
mbinguni kwa shangwe.
Nimrudishie roho
Mwokozi Bwanangu,
aipokee vema,
aipe uzima.
3 Mara moja roho itakwenda
kufika mbinguni,
ikiacha uzima wa hapa
kwa nguvu ya Mungu.
Yapelekwa na gari
kama Eliya mkuu,
malaika waibeba
vizuri kwa shangwe.
4 Nikifika kule Paradiso,
mwisho huu ni mwema.
Roho yangu yajaa furaha
kinywa husifu tu.
Wateule huimba
nyimbo nzuri nyingi,
hawaachi kumsifu
Mungu Mwenye enzi.
Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #155