1 Tuimbe na kusifu
kwa nyimbo za furaha:
Yesu Bwana wetu
amezaliwa leo
zizini Betlehemu,
furaha ya mioto.
Mponya na Mwokozi,
tunakusifu.
2 Nakutamani sana,
uliyetoka juu.
Ee Mowokozi mwema
tuliza moyo wangu,
unipe neema yako,
Mtoto wa huruma.
Univute juu, univute juu.
3 Rehema zake Mungu
ni nyingi, alimtuma
Mwana wake Yesu,
awakomboe watu,
atufanyie njia,
tufike tena kwetu.
Kwetu ni kwa Mungu,
kwetu kwa Mungu.
4 Na watu wakaao
katika giza wote
wanakungojea
wewe Mowokozi wetu,
na kukufurahia
uliyetukomboa.
Yesu Bwana wetu
twakutukuza.
Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #17