1 Shujaa mkubwa, Bwana wetu,
leo umejikalisha
kitini kwa Babako.
Ufalme wote ni wako,
umeshinda maadui,
hawanna nguvu tena.
Umepewa enzi kubwa,
kufa pia na uzima,
vyote unavitawala.
2 Malaika wote wa mbingu
wanakusifu kwa nyimbo,
wanakutumikia.
Ulipotoka mbinguni
ukaja kutuokoa,
na umerudi leo.
Sasa, wako utukufu;
nasi tunakushukuru,
tunasifu jina lako.
3 Twataka kutafuta tu
ufalme wako wa mbingu.
Utupe nguvu zako,
tushike mwenendo mwema,
tushiwe wenye kiburi
ila wanyenyekevu.
Tuepuke kila kosa,
tufuate njia yako
ya kuingia mbinguni.
4 Yesu mwana wa Daudi
uliyetupatanisha
na Bwana Mungu wetu.
Ulipokwenda mbinguni
umetutengenezea
makao ya milele.
Tuongoze, tusichoke,
tusafiri siku zote;
kwani watungoja kwako.
Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #121