1 Nimshangilie Bwana wangu
na kumwimbia mkombozi,
katukomboa msalabani,
nisifu pendo lake kuu.
Haya mwimbieni Yesu,
amekubali mateso,
katukomboa msalabani,
tusifu pendo lake kuu!
2 Tumsifu yeye mponya wetu
katika ulimwengu huu,
kutupatanisha na Baba
walio wakosaji tu.
Haya mwimbieni Yesu,
amekubali mateso,
katukomboa msalabani,
tusifu pendo lake kuu!
3 Katuletea mwanga wake,
tulikaa katika giza,
wokovu ukaonekana,
kamshinda mwovu, ni shujaa!
Haya mwimbieni Yesu,
amekubali mateso,
katukomboa msalabani,
tusifu pendo lake kuu!
4 Na tumtukuze Bwana wetu,
tumtumikie kwa bidii,
na atawale apendavyo,
na sisi sote tutamtii!
Haya mwimbieni Yesu,
amekubali mateso,
katukomboa msalabani,
tusifu pendo lake kuu!
Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #83