Author: E. A. Hoffman Hymnal: Mwimbieni Bwana #165 (1988) First Line: Wamwendea Yesu kwa kusafishwa Lyrics: 1 Wamwendea Yesu kwa kusafishwa,
Na kuoshwa kwa dau ya Kondoo!
Je, neema yake umemwagiwa?
Umeoshwa kwa damu ya Kondoo?
Kuoshwa, kwa damu
Itutakasayo ya Kondoo;
Ziwe safi nguo nyeupe mno;
Umeoshwa kwa damu ya Kondoo?
2 Wamwandama daima Mkombozi
Na kuoshwa kwa damu ya kondoo?
Je, waishi kwake msulibiwa?
Umeoshwa kwa damu ya Kondoo?
Kuoshwa, kwa damu
Itutakasayo ya Kondoo;
Ziwe safi nguo nyeupe mno;
Umeoshwa kwa damu ya Kondoo?
3 Atakapokuja Bwana arusi
Uwe safi kwa damu ya Kondoo!
Yafae kwenda Mbinguni mavazi
Yafuliwe kwa damu ya Kondoo.
Kuoshwa, kwa damu
Itutakasayo ya Kondoo;
Ziwe safi nguo nyeupe mno;
Umeoshwa kwa damu ya Kondoo?
4 Yatupwe yaliyo na takataka,
Na uoshwe kwa damu ya Kondoo.
Huoni kijito chatirika
Na uoshwe kwa damu ya Kondoo?
Kuoshwa, kwa damu
Itutakasayo ya Kondoo;
Ziwe safi nguo nyeupe mno;
Umeoshwa kwa damu ya Kondoo? Topics: Ubatizo Languages: Swahili
Wamwendea Yesu