Hymnal: Mwimbieni Bwana #117 (1988) First Line: Mle kaburini Refrain First Line: Bwana! Amefufuka Lyrics: 1 Mle kaburini, Yesu Mwokozi
Alilazwa chini, Bwana wangu!
Refrain:
Bwana! Amefufuka,
Kifo kimeshindwa kabisa!
Gizani mle alitoka chini,
Sasa atawala huko Mbinguni!
Yu hai! Yu fai!
Bwana Yesu yu hai.
2 Aungoja huo, Yesu Mwokozi!
Mchana ujao, Bwana wangu! [Refrain]
3 Walinda kaburi, Yesu Mwokozi!
Bure ni muhuri, Bwana wangu! [Refrain]
4 Kifo kimeshindwa, Yesu Mwokozi!
Pingu zimevunjwa, Bwana wangu! [Refrain] Topics: Yesu amefufuka Languages: Swahili
Mle kaburini, Yesu Mwokozi