Instance Results

‹ Return to hymnal
Hymnal, Number:nziy1994
In:instances

Planning worship? Check out our sister site, ZeteoSearch.org, for 20+ additional resources related to your search.
Showing 1 - 10 of 308Results Per Page: 102050
TextPage scan

Baba, Mwana Roho

Hymnal: NZIY1994 #2 (1994) First Line: Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi Lyrics: 1 Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi, Kila tukiamka tunakuabudu. Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi, Ewe Utatu, tunakusifu. 2 Baba, Mwana, Roho, wakuaminio, Wanakutolea shukurani zao. Wakusujudia malaika nao: Wewe U mwanzo, nawe U mwisho. 3 Baba, Mwana, Roho, sisi tu gizani, Utukufu wako makosa hauna, U Mtakatifu, nawe U mapenzi, U peke yako, mwenzio huna. 4 Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi, Ulivyoviumba vyote vyakusifu: Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi, Ewe Utatu, tunakusifu. Topics: Irada, Sifa Na Injil Scripture: Isaiah 6:3 Languages: Swahili
Text

Watu Wa Yesu

Hymnal: NZIY1994 #3 (1994) First Line: Watu wa Yesu, sifuni Bwana Lyrics: 1 Watu wa Yesu, sifuni Bwana, M-tangazeni, ulimwenguni, Sifa za Yesu, zienee pote, Mataifa yote, yamsifu Yesu. 2 Humilki pote, mbingu na n-chi, Ufalme wake, hauna mwisho, Wote wa mbinguni m-tukuzeni, Msifuni daima hata milele. 3 Neema yake ni nyingi sana, Upendo wake ni wa ajabu, M-linzi, M-chunga,Mwokozi wetu Mfarifi, Mwombezi na Kiongozi. 4 Fadhili zake zaonekana, Anavikidhi viumbe vyake, Vyakula, vinywaji ni vingi kwake, Mwangaza na mvua atugawia. 5 Sifuni Bwana kamwimbieni, Anastahili fahari yoge, Heshima na pendo m-peni Bwana, Mwokozi Mwombezi na Mfalme Yesu. Topics: Irada, Sifa Na Injil Scripture: Psalm 104:1 Languages: Swahili
Text

Mungo Mtukufu Aleye Bwana

Hymnal: NZIY1994 #4 (1994) First Line: Mungu M-tukufu aliye Bwana Refrain First Line: Msifuni, msifuni, nchi imsikie Lyrics: 1 Mungu M-tukufu aliye Bwana, Akamtoa Yes Mwana M-pendwa; Akawa dhabihu kwa dhambi zote, Kufungua njia kwa watu wote. Refrain: Msifuni, msifuni, nchi imsikie: Msifuni, msifun, Bwna mshangilie: Njoni kwake Baba kwa Yesu Mwana, M-peni heshima aliye Bwana. 2 Ukombozi wetu, tendo la Mungu, Ni ukamilifu kwa kila m-tu; Mwenye ukosefu akimwamini, Atasamehewas na Yesu, kweli. [Refrain] 3 Ametufundisha mambo ya mbingu, Tukafurahiswa na Mwana Mungu; Ametuinua tukae naye, Atatuongoza hata milele. [Refrain] Topics: Irada, Sifa Na Injil Scripture: Galatians 1:4-5 Languages: Swahili

Msifu Mungu

Author: M. G. Mutsoli Hymnal: NZIY1994 #5 (1994) First Line: Haleluya msifu Mungu, katifa patakatifu Topics: Irada, Sifa Na Injil Scripture: Psalm 150 Languages: Swahili

Mungu Ni Pendo

Hymnal: NZIY1994 #6 (1994) First Line: Mungu ni pendo, apenda watu Topics: Irada, Sifa Na Injil; Upendo Wa Mungu Scripture: John 3:16 Languages: Swahili
TextPage scan

Ni Siku Tukufu

Hymnal: NZIY1994 #7 (1994) First Line: Ni siku tukufu, Haleluya, amina Lyrics: 1 Ni siku tukufu, Haleluya, amina, Ya kupumzika, Haleluya, amina, Tuache shughuli, Tumwabudu Mungu, Bwana wa mbinguni, Haleluya, amina. 2 Ni siku tukufu, Haleluya, amina, Tukufu kabisa, Haleluya, amina, Njoni ndugu zangu, Tumwabudu Mungu, Kwa roho na kweli, Haleluya, amina. 3 Ni siku tukufu, Haleluya, amina, Ya furaha mno, Haleluya, amina Yesu kafufuka, Na sasa y hai, Anatuombea, Haleluya, amina. 4 Ni siku tukufu, Haleluya, amina, Ndiyo maarufu, Haleluya, amina, Tunaye Mwokozi, Agukoaye, Sasa na milele, Haleluya, amina. 5 Ni siku tukufu, Haleluya, amina, Siku ya neema, Haleluya, amina Tangazeni Neno,La Bwana Mwokozi, Msifuni daima, Haleluya, amina Topics: Irada, Sifa Na Injil Scripture: Psalm 96:2 Languages: Swahili
TextPage scan

Zaburi 100

Hymnal: NZIY1994 #8 (1994) First Line: Imbeni nyote sifa za Bwana Lyrics: 1 Imbeni nyote siva za Bwana, Na njoni kwake, Ee dunia. Shangelieni nyote pamoja, Atumkiwe kwa furaha. 2 Bwana ni Mungu, jueni nyote; Alituumba, si wenyewe, Na sisi sote tu watu wake, Tu kondoo wake sisi sote. 3 Nyuani mwake na malangoni, Ingieni na usukuru. Mshukuruni, shangilieni, Na jina lake lisifuni. 4 Kwa kuwa wema ni wake Mungu, Hata milele ni karimu. Uaminifu wa Bwana wetu, Vizazi vyote utadumu. Topics: Irada, Sifa Na Injil Scripture: Psalm 100 Languages: Swahili
Text

Jina La Yesu Sifuni

Hymnal: NZIY1994 #9 (1994) Lyrics: 1 Jina la Yesu sifuni, viumbe vya Mungu, Wa mbinguni na n-chini, Yesu mwabunduni, Wa mbinguni na n-chini, Yesu mwabunduni. 2 Watokao hukumuni shukuruni sana, Awarehemuye wote, Yesu mwabuduni, Awarehemuye wote, Yesu mwabuduni. 3 Kristo alisulibiwa kwa ajili yetu, Mpendeni, waokokao, Yesu mwabuduni, Mpendeni, waokokao, Yesu mwabuduni. 4 Wa falme zote n-chini, m-sujudieni, Mwimbieni Mfalme wetu, Yesu mwabuduni, Mwimbieni Mfalme wetu, Yesu mwabuduni,. 5 Watampigia magoti wafalme wote, Na ninyi waaminifu, Yesu mwabuduni, Na ninyi waaminifu, Yesu mwabuduni Topics: Irada, Sifa Na Injil Scripture: Revelation 5:13 Languages: Swahili

Bariki Baba

Author: M. G. Mutsoli Hymnal: NZIY1994 #10 (1994) First Line: Bariki, bariki Baba Topics: Irada, Sifa Na Injil; Sadaka Scripture: Psalm 115:13 Languages: Swahili
TextPage scan

Jina La Yesu, Salamu!

Hymnal: NZIY1994 #11 (1994) First Line: Jina la Yesu, salamu! Refrain First Line: Na enzi, enzi Lyrics: 1 Jina la Yesu, salumu! Lisujudieni, Lisujudieni; Ninyi mbinguni, hukumu, Na enzi, enzi, enzi, enzi, Enzi enzi, enzi na enzi mpeni. 2 Enzi na apewa kwenu, Wateteea dini, Watetea dini; Mkuzeni Bwana wenu Na enzi, enzi, enzi, enzi, Enzi enzi, enzi na enzi mpeni. 3 Enyi mbegu ya rehema, Nanyi msifuni, Nanyi msifuni; Mmeponywa kwa neema, Na enzi, enzi, enzi, enzi, Enzi enzi, enzi na enzi mpeni. 4 Wenye dhambi kumbukeni, Ya msalabani, Ya msalabani, Kwa furaha msifuni, Na enzi, enzi, enzi, enzi, Enzi enzi, enzi na enzi mpeni. 5 Kila mtu duniani Msujudieni, Msujudieni; Kote-kote msifuni, Na enzi, enzi, enzi, enzi, Enzi enzi, enzi na enzi mpeni. 6 Sisi na wao pamoja tu Humo sifani, Humo sifani; Milele sifa ni moja, Na enzi, enzi, enzi, enzi, Enzi enzi, enzi na enzi mpeni. Topics: Irada, Sifa Na Injil Scripture: Matthew 1:21 Languages: Swahili

Pages


Export as CSV