15. Watu Wote Duniani

1 Watu wote duniani, Mwimbieni Mungu wetu,
M-cheni na kumsikia, Njoni kwake na furaha.
M-cheni na kumsikia, Njoni kwake na furaha.

2 Milima, bahari zote, Nyota nazo,jua pia,
Na vyote alivyoumba, M-sifuni Mungu wenu.
Na vyote alivyoumba, M-sifuni Mungu wenu.

3 Muumba ni Mungu peke, Wa watu na vitu vyote,
Mwenyezi nchini na juu, Ndiye M-linzi wa watu.
Mwenyezi nchini na juu, Ndiye M-linzi wa watu.

4 Tumfurahie daima, Tumkaribie kitini,
Anao uzima kweli, Ndiye Mchungaji wa wote.
Anao uzima kweli, Ndiye Mchungaji wa wote.

5 Tumsifuni siku zote, Kwa shukrani tumwimbie,
Atutawale daima, Kwa wingi, wa neema yake.
Atutawale daima, Kwa wingi, wa neema yake.

Text Information
First Line: Watu wote duniani
Title: Watu Wote Duniani
Language: Swahili
Publication Date: 1994
Scripture:
Topic: Irada, Sifa Na Injil
Notes: Sauti #1: Doxology (Old 100th): (Baptist Hymnal 1991 #253, Nyimbo za Sifa #18) Mlio wa G - Mapigo 4/4; Sauti #2: by David Makathimo (© 1994 David Makathimo) Mlio wa G - Mapigo 3/4
Tune Information
(No tune information)

Suggestions or corrections? Contact us