Text: | Bwana imepita tena |
Author: | K. Neumann, 1648-1715 |
1 Bwana, imepita tena
siku moja ya neema.
Nifundishe nifikiri
mambo yote ya leo.
Unionyeshe sasa
niliyokukosea.
Nimalize mambo yote
kadiri ya mapenzi yako.
2 Kweli utaona mengi
yasiyokupendeza,
Kwani ni mtu wa makosa,
yaliyo mengi sana.
Moyo wangu, na kinywa,
na mikono ya kosa
kwa kuwaza na kusema
na kutenda kila siku.
3 Nakuomba ewe Mungu
nihurumie tena.
Ondoa maovu yote
niliyokutendea.
Uyafute makosa
kwa rehema yako kuu.
Nitaangelia kesho
nizishike amri zako.
4 Bwana wewe unakesha,
sisi tukisinzia.
Macho yakk hayachoki,
ndiwe mchungaji mwema,
awalindaye kondoo
katika giza lote.
Utulinde sisi sote,
kondoo wako tulalapo.
5 Kukipambazuka tena
niondoke kwa bidii
nikutumikie vema
katika mambo yote;
utakaponiita
nife leo usiku,
ninakuwekea Bwana,
roho mikononi mwako.
Text Information | |
---|---|
First Line: | Bwana, imepita tena |
Title: | Bwana imepita tena |
German Title: | Herr, es ist von meinem Leben |
Author: | K. Neumann, 1648-1715 |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Kumtambikia Mungu: Nyimbo za Jioni |
Notes: | Sauti: Werde munter, mein Gemüte by J. Schop, 1642, Posaunen Buch, Erster Band #69, Nyimbo za Kikristo #172 |