181. Nuru ya roboni

1 Nuru ya rohoni ni Bwana Yesu.
Nakuomba sana: Niangazishe;
ukanitazame kwa huruma tu
Ukanitulize mimi maskini,
Ukanitulize mimi maskini.

2 Futa dhambi zangu kwa damu yako.
Hasira ya Mungu iniondoke.
Machubuko yako, hata mateso,
Niyawaze vema rohoni mwangu,
Niyawaze vema rohoni mwangu.

3 Nakutumaini peke yako tu.
Niwe mtumwa wako pote nilipo.
Utanikubali, sina mashaka!
Nitakushukuru pasipo mwisho,
Nitakushukuru pasipo mwisho.

Text Information
First Line: Nuru ya rohoni
Title: Nuru ya roboni
German Title: Jesu, Gnadensonne
Author: G. Knak, 1806-1873
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Chakula cha Bwana
Notes: Sauti: Freiheit, die ich meine by Groos, 1818, Posaunen Buch XXII (353), Reichs Lieder #182
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us