174. Heri kumjua Yesu, Bwana

1 Heri kumjua Yesu Bwana
Roho huamka, aniita.
Anitambua mali yake,
hanipotezi. Niko kwake.
Msimuliwe sifa zake.
Hana mwenzake,
Mponya pekee
afurahisha moyo kweli
Yeye ni Yesu, tumtukuze.

2 Nikimwambia mambo yote
anituliza moy vema.
Nikimfanyia kazi zangu,
anibariki hapa na juu.
Msimuliwe sifa zake.
Hana mwenzake,
Mponya pekee
afurahisha moyo kweli
Yeye ni Yesu, tumtukuze.

3 Nikimjutia nimekosa,
anaondoa na mashaka.
Yeye hapendi nikishindwa,
anipa nguvu za kwendea.
Msimuliwe sifa zake.
Hana mwenzake,
Mponya pekee
afurahisha moyo kweli
Yeye ni Yesu, tumtukuze.

Text Information
First Line: Heri kumjua Yesu Bwana
Title: Heri kumjua Yesu, Bwana
English Title: Blessed assurance
Author: F. J. Crosby, 1880-1915
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Notes: Sauti: Blessed assurance by J. F. Knapp, 1820-1915, Sacred Songs and Solos #873, Reichs Lieder #237
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us