167. Shika mikono yangu

1 Shika mikono yangu, niongoze,
mpaka nimalizapo safari hii.
Nikiwa peke yangu napotea.
Popote uendapo nipeleke!

2 Tuliza moyo wangu, uwe kimya,
nikiona furaha au majonzi,
unitulize sana, ndimi wako,
sitaki neno tena, ila hilo.

3 Nisipoona leo nguvu yako,
najua wanilinda, huniachi,
Shika mikono yangu niongoze,
mpaka nimalizapo safari hii!

Text Information
First Line: Shika mikono yangu, niongoze
Title: Shika mikono yangu
German Title: So nimm denn meine Hände
Author: J. Hausmann (1877)
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kipaimara
Notes: Sauti: Wie könnt ich ruhig schlafen by F. silcher, Tübingen 1342, Posaunen Buch XXV (358), Reichs Lieder #648, Lutheran Book of Worship #353
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us