Text: | Bwana twakuletea |
Author: | B. Schmolk, 1672-1737 |
1 Bwana, twakuletea
mtoto huyu, tukijua
(watu hawa, tukijua)
amri yako ya mwisho
uliyowapa mitume:
Watu wote wabatizwe,
watakaokuwa wako.
2 Neno hili ni kubwa
tulilopewa na Yesu:
Atakaye kufika
katika ufalme wako,
hana budi kuzaliwa
tena kwa maji na Roho.
3 Pokea kondoo wako
mchunga mwema Bwana Yesu.
Umwongoze mbinguni.
(Waongoze mbinguni,)
ndiwe njia na uzima.
Umpe kukutegema.
(wape kukutegemea,)
apate kutengemana.
(wapate kutengemana.)
4 Baba, tunakushi
ukubali wimbo wetu,
usikie maombi
tunayokuyomba sasa.
Andika jina la mtoto,
(Andika majina yao)
katika kitabu chako!
Text Information | |
---|---|
First Line: | Bwana, twakuletea |
Title: | Bwana twakuletea |
German Title: | Liebster Jesu, wir sind hier |
Author: | B. Schmolk, 1672-1737 |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Ubatizo |
Notes: | Sauti asili: Ja er ist's das Heil der Welt by J. R. Ahle, 1664, Posaunen Buch #32 |