Text: | Ninapenda kwenda zangu |
Author: | L. Knak, 1806-1878 |
1 Ninapenda kwenda zangu
nimwone Mwokozi wangu.
Moyo wangu watamani
kuambatana na Yesu
na kumsifu milele,
na kumsifu milele.
2 Ninapenda kusikia
nyimbo za malaika wote.
Ningekuwa na mabawa
ningeruka leo hivi
mpaka Sayuni kwake,
mpaka Sayuni kwake.
3 Ninapenda kuingia
pale penye utukufu,
penye nyumba za dhahabu
nimwone Mwokozi wangu
na furaha za mbinguni,
na furaha za mbinguni.
4 Ninapenda kuuona
uzuri wa Paradiso.
Nikifika nitapata
tunda lake tamu sana,
Yesu, nipeleke juu!
Yesu, nipeleke juu!
Text Information | |
---|---|
First Line: | Ninapenda kwenda zangu |
Title: | Ninapenda kwenda zangu |
German Title: | Lass mich gehen |
Author: | L. Knak, 1806-1878 |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Yesu amepaa mbinguni |
Notes: | Sauti: Lass mich gehen by F. L. Werman, Dresden, 1879, Posaunen Buch XXIV #356 |