124. Tazameni anapaa

1 Tazameni, anapaa,
mwenye kushinda vita;
Gari lake ni mawingu,
ndipo anapopita;
Malaika wa mbinguni
wakimwimbia Bwana;
Amekaribishwa sana,
kwa kufurahi sana.

2 Ni nani anayepaa,
wote wakimsifu?
Ndiye Bwana mwenye enzi,
ndiye Mungu wa Safu,
Aliyeteseka kwanza mle
katika Mti,
Kwa kifo chake mwenyewe,
akashinda mauti.

3 Akaaga watu wake,
akiwabarikia,
Akapanda mawingunyi,
wakimtazamia,
Chini hutenda ya Mungu,
yote yakatimia;
Kazi yake imekwisha,
kwake amerejea.

4 Ni Kuhani wetu sasa,
yumo na damu yake,
Katika Patakatifu
twapatanishwa kwake;
Amefanya ukombozi,
kuondoa dhambi zetu;
Mungu amemkubali,
ndiye sadaka yetu.

5 Mwili ameuinua huo wa
ki-Adamu,
Ndani yake sisi sote
pia tuna sehemu,
Mungu na mtu pamoja
yuko huko enzini
Twaamini Bwana, kwamba
tutakwenda mbinguni.

Text Information
First Line: Tazameni, anapaa
Title: Tazameni anapaa
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Yesu amepaa mbinguni
Notes: Asili ya wimbo: Nyimbo Standard #187, Sauti ya wimbo: Sacred Songs and Solos #157
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us